Thursday, 16 April 2015


Floyd Mayweather akifanya mazoezi mtaani na kuruhusu apigwe picha.
Katika hali isiyotarajiwa bondia raia wa Marekani Floyd Mayweather ameamua kufanya mazoezi ya wazi na kuruhusu vyombo vya habari kuchukua picha ikiwa ni maandalizi kuelekea katika pambano lake dhidi ya bondia Manny Pacquiao raia wa Philippine.
Mayweather ambaye ni bingwa wa WBA na WBC, ameweka rekodi ya kucheza mapambano 47 ya kulipwa bila kupoteza hata moja wakati mpinzani wake amepigana mapambano 57, akiwa amepigwa mara tano na kutoka sare mara mbili.
Pambano kati ya wawili hao linatarajiwa kufanyika mnamo May 2 mwaka huu, huku pigano hilo likitajwa kuwa ndio la pesa nyingi zaidi katika historia ya ngumi duniani.

0 comments:

Post a Comment