Yanga imezidi kuchanja mbuga kuelekea katika ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuwafunga Mbeya City 3-1 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga ndio wawakilishi wa Tanzania bara pekee waliobaki katika michuano ya vilabu ya Afrika baada ya Azam kutolewa na El-Merreikh ya Sudan na ushindi mfululizo inaoupata katika mechi zake ni kama vile kutuma salamu kwa Etoile du Sahel ya Tunisia, ambayo itacheza na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania katika mechi ya Shirikisho Afrika hatua ya 16 bora.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Liberia, Kpah Sherman amefunga goli moja (dakika 19) , huku magoli mengine yakitoka kwa Salum Telela (dakika 39) huku Felix Themi akifunga goli la kufutia machozi kwa City dakika 41). Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” alifunga goli la tatu dakika 5 baada ya kipindi cha pili, ambacho Mbeya City walibaki wachezaji 10 uwanjani dakika 57 baada ya Themi kutolewa kwa kile knachodhaniwa kutoa lugha mbaya kwa mwamuzi wa mchezo.
Kwa ushindi huo, Yanga inazidi kujukita kileleni ikiwa na pointi 46 ikifuatiwa na bingwa mtetezi, Azam ikiwa na pointi 38, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar hivi karibuni
0 comments:
Post a Comment