Dereva nambari moja duniani Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes ameibuka bingwa kwa mara nyingine katika shindano la Grand Prix lililofanyika huko China. Hamilton aliendesha kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata ubingwa huo huku mchezaji mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg akikamata nafasi ya pili.
Hata hivyo Rosberg amemlalamikia Hamilton kwa kujaribu kumrudisha nyuma katika kumkimbiza Sebastain Vettel wa timu ya Ferrari, madai ambayo yanapingwa vikali na Hamilton.
Nafasi ya tatu imeenda kwa Sebastain Vettle huku ya nne ikiangukia kwa Kimi Raikkonen wote kutoka timu ya Ferrari.
0 comments:
Post a Comment