Miamba ya jiji la Madrid nchini Hispania, Atletico Madrid na Real Madrid zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya,UEFA, hatua ya robo fainali.
Atletico ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huu, uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon, ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Bernabeu tarehe 22 Aprili.
Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale alikosa nafasi muhimu mapema katika dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza cha mchezo kwa kushindwa kutumbukiza mpira wavuni. Hata hivyo kikwazo alikuwa mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak, ambaye alinga'ara katika mchezo huo kwa kupangua michomo mikali ya wachezaji wa Real Madrid wenye uchu wa magoli kama vile James Rodriguez, huku naye Mario Suarez wa Atletico Madrid akikosa nafasi ya kuifungia timu yake mwishoni mwa mchezo huo.
Real Madrid inalenga kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa wa kombe hilo mfululizo kwa kulitwaa tena mwaka huu baada ya kulitwaa mwaka 2014kama ilivyowahi kufanya AC MIlan ya Italia mwaka 1989 na 1990, ikih
Mlinda mlango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas amemzidi mchezaji wa Barcelona, kwa kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi katika michuano hiyo kwa kucheza mechi 147.
Vijana wa Carlo Ancelotti ni mchezo wao wa saba kukutana na Atletico Madrid bila kushinda.
Mchezo mwingine uliochezwa jana usiku ulizikutanisha Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa. Matokeo ni kwamba Juventus imeibuka na ushindi wa goli 1-0. Juventus ilipata bao lake pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti ikifungwa na Vidal. Juventus inalenga pia kufika hatua ya nusu fainali ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003. Hata hivyo kocha wa Monaco Leonardo Jardim, ameilalamikia penalti hiyo kuwa haikuwa ya haki. Timu hizi nazo zitarudiana huko Monaco Aprili 22.
Michezo mingine miwili ngazi ya robo fainali itakayopigwa Jumatano itazipambanisha FC Porto ya Ureno dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, huku Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiikaribisha Barcelona ya Hispania.
0 comments:
Post a Comment