Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Jumatano katika viwanja viwili nchini Tanzania, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Azam itakuwa katika jitihada za kujaribu kutetea ubingwa baada ya kutoa droo katika mechi zake mbili zilizopita, hivyo kuipa nafasi Yanga.Azam, ambao ndio mabingwa watetezi, wana pointi 38 huku Yanga wakiongoza ligi kwa pointi 46.
Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.
0 comments:
Post a Comment