Katika kile kinachoonekana ni kuweka mikakati ili kuchukua ubingwa msimu ujao, wekundu wa Msimbazi, Simba inahaha kutafuta wachezaji
kutoka nje ya nchi ili kuimarisha kikosi chake.
Hatua hiyo inakuja baada ya Simba, iliyomaliza ya tatu katika msimu wa
ligi iliyopita, kuripotiwa kuachana na wachezaji watatu wa kigeni kutoka Uganda, Simon Sserunkuma, Dan Sserunkuma na Joseph Owino
kufuatia pendekezo la kocha Mserbia Goran Kopunovic.Habari kutoka Simba zinasema sasa ni wakati wa kutafuta wachezaji
katika nchi jirani za Afrika ili kuziba pengo la Waganda hao.
Baachi ya nchi ambazo zimeelezwa kuwa Simba inasaka wachezaji ni
pamoja na Ghana, Nigeria, Rwanda, Burundi na Kenya.Uamuzi huo unakuja baada ya Simba kuwe nje ya michuano ya kimataifa
kwa takriban miaka mitatu mfululilizo.Ligi kuu ya Tanzania Bara imekwisha hivi karibuni huku Yanga ikiwa
bingwa na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam kumaliza nafasi ya pili.
Yanga na Azam ndio wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya
vilabu ya CAF hapo mwakani.Yanga itashiriki kombe la Washindi barani Afrika na Azam itashiriki kombe la Shirikisho.
0 comments:
Post a Comment