Thursday, 16 April 2015


hambulizi lililosababisha kifo cha Rafik Hariri
Mwaandishi habari mmoja raia wa Lebanon leo atakuwa mshtakiwa wa kwanza kufikishwa kizimbani katika mahakama ya jinai ya ICC iliyoko The Hague nchini Uholanzi katika uchunguzi wa kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri.
Bi Karma Khayat na runinga anayoifanyia kazi ya Al-Jadeed, yanashutumiwa kwa kupuuza ushauri wa kundi maalum la uchunguzi wa kesi hiyo nchini Lebanon, kwa kutoa taarifa kuwahusu mashahidi.
Amekanusha kutenda kosa lolote.
Bi Khayat anashutumiwa kwa kutoa taarifa kuwahusu mashahidi katika kesi ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik Hariri.
Bi Khayat amesema kuwa ripoti yake ilikuwa kwa manufaa ya uma.
Mahakama hiyo maalum ilibuniwa na umoja wa mataifa, ili kubaini watu waliohusika na mauaji ya bwana Hariri.
Watu watano wanaotuhumiwa kuhusika katika mauwaji hayo ya Hariri wangali mafichoni.

0 comments:

Post a Comment