This is featured post 1 title
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgan1RFf60ForospUB-yYR1zLtop_M6KgLtKHuEaQZp5MSv6L1nJt6WpPaotUMk7WTPWiGfAzqD7ISb-knHwH3bRj9UNkkNyp-6_uR3yeOPCjkNEVvUEL6jgP9ZjWnz6CDLhis9I6kijPw/s1600/DSC_0000047.jpg)
This is featured post 2 title
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFWH61LnGSFkBLf-F5yhz7h9xFL89UTicjHH3uZOeC_gyBUqFYbInlLl3We4DE9beL-hUggPrTB4NwfU-nQz6LzJfXWkE0JfcR9ypTdmDWxkL9SdJdawpZV5zAUABuu45uzuLnHbJZh7Y/s1600/DSC_0000087.jpg)
This is featured post 3 title
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghvt4Bq6oMu2vQJ-875hyphenhyphenYTdrdlbEhB-KD2zs0ogMgya4k1FY9ZlEWzomzp6dRmAbiGyeWxqkW-KKpG7wIvoLqcMlW3MvcHNdpynK9AFYF-ZppzrbU6Y6E7twSJlZCWmq3N26cL1Modes/s1600/DSC_0000086.jpg)
Thursday, 23 April 2015
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.
Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Volcano aina ya Calbuco imelipuka kwa muda mfupi huko ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 40.
Watu waliokuwa wakiishi maeneo jirani na ulikotokea mlipuko wa Volcano hiyo wamelazimika kuyahama makazi yao.
Picha za televisheni zilionyesha wingu zito na majivu vikipanda hewani umbali kilomita kadhaa angani katika jimbo la Los Lagos kusini mwa Chile.
Mamlaka nchini humo zimetoa tangazo la hali ya hatari kwa wakazi wote ambao wapo umbali wa kilomita la mlipuko wa Volcano hiyo huku safari za ndege kuelekea eneo hilo zikiwa zimeahirishwa.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Marekani imeilaumu Urusi kwa kuweka mfumo kujihami na mashambulizi ya anga Mashariki mwa Ukraine,hali ambayo ni kinyume na makubaliano yaliyosainiwa mwezi Februari mwaka huu.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Marekani Bi. Marie Harf, amesema hatua ya majeshi ya Urusi kujenga mifumo ya ulinzi wa anga karibu na eneo la mapigano ni kinyume na makubaliano. Harf pia ameishutumu Urusi kwa kupeleka vikosi zaidi vya wanajeshi katika eneo hilo na kuendesha mafunzo kwa makundi yanayoipinga serikali. Hata hivyo Urusi haijajibu lolote kutokana na tuhuma hizo za Marekani,lakini awali Urusi iliwahi kukanusha kuwa haina vikosi vya majeshi ndani ya Ukraine.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini Yemen, huku Mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha siku tisa zilizopita.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni upelekaji wa huduma za kitabibu.
Awali Saudi Arabia ilisema itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande mbili.
Monday, 20 April 2015
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Kundi la wapiganaji wadola ya Kiislam IS limetoa video inayo onyesha mauaji ya zaidi ya watu 30 raia Ethiopia ambao ni Wakristo wakiuawa wengine kwa kuchinjwa katika ufukwe wa bahari na wengine kwa kupigwa risasi kichwani jangwani. Hata hivyo video hiyo inabainisha wazi kwamba kundi hilo la IS linawaua watu hao kwa sababu ni wakristo. Serikali ya Ethipia imesema kuwa inajaribu kufuatilia utambulisho wa utaifa wa watu hao kupitia ubalozi wa Cairo nchini Misri. Hali ya usalama nchini Libya imetetereka tangu kuangushwa kwa utawala wa Kanal Muamar Gadaf, ambapo pia ustawi wa kundi la kigaidi wa wapiganaji wa dola ya Kiislam umekuwa mkubwa.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Aston Villa imetinga fainali ya kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 baada ya Fabian Delph kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Liverpool katika mechi ya semi fainali.
Ushindi huo umeiwacha Liverpool bila kitu msimu huu .
Liverpool ilichukua uongozi kupitia Phillipe Coutinho ambaye alivamia lango la Aston Villa kabla ya kucheka na wavu licha ya kukabwa na wachezaji wa Villa.
Lakini Villa walisawazisha kupitia Christian Benteke aliyepata pasi kutoka kwa Delph.
Delph baadaye alifunga bao la pili baada ya kuwapita walinzi wa Liverpool na hivyobasi kutinga fainali ya kombe hilo na Arsenal mnamo tarehe 30 ilioicharaza Reading 2-1 siku ya jumamosi.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Baada ya Aston Villa kushinda bao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mechi ya nusu Fainali michuano ya FA Cup,sasa kocha wa Aston Villa Tim Sherwood anasema wanajinoa kuwakabili Arsenal katika mechi ya fainali.
Hata hivyo amesema kuwa wanatakiwa kujiandaa vilivyo kwani Arsenal katika mechi za awali walizocheza nao waliwahi walipewa kipigo cha 3-0 na 5-0 hivyo akasema maandalizi wanayopaswa kuyafanya si ya mzaha.
Sherwood amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kufanyika ya maandalizi kuanzia sasa hadi siku ya May,30mwaka huu.
Tutakachotakiwa kukifanya nikujilinda,lakini wakati huo huo kushambulia na kuhakikisha tunawashinda Arsernal.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Rais wa China Xi Jinping ameanza ziara ya siku mbili nchini Pakistan hii leo.
Bwana Xi atazindua mpango wa uwekezaji wa kichina wa gharama ya dola bilioni 50 ambao Pakistan ina matumaini kuwa utasuluhisha tatizo lake ya nishati.
Mpango huo unaofahamika kama barabara ya uchumi ya China na Pakistan ni pamoja na barabara , reli na mabomba ya jumla ya umbali wa kilomita 3000 kutoka mji wa bandari wa Gwadar nchini Pakistan hadi mji wa ulio mashariki mwa China wa Kashgar.
Waandishi wa habari wanasema kuwa lengo la China ni kuongeza ushawishi wake wa kiuchumi kwa Pakistan ili kulegeza ule wa Marekani na India.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji wanaoangamia kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia ajali ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha Lampedusa, nchini Italia.
Manusura 28 wa janga la hivi punde kwenye bahari ya Meditaranean walitarajiwa kufikishwa kisiwani Sicily alfajiri ya Jumatatu. Hadi kufikia usiku, ni miili 24 iliyokuwa imeopolewa, na maafisa wa usalama kwenye pwani ya Italia, wakaipeleka kisiwani Malta.
Ni vigumu kuhakikisha idadi ya watu walioanza safari kwenye boti hiyo kutoka pwani ya Libya. Lakini walionusurika wanasema walikuwa kati ya watu 500 na 700 kabla ya kupinduka kilomita mia mbili kutoka Lampedusa, kwenye maji ya Libya.
Ikiwa idadi hiyo itathibitishwa basi hii itakuwa ndio ajali mbaya zaidi kati ya nyingi ambazo zimekuwa zikitokea karibuni kwenye bahari ya mediteranean, huku watu wakifanya safari za hatari kutafuta maisha bora ulaya.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amesema zaidi ya mawakala 900 wa kusafirisha watu wamekamatwa. Alisema suluhu la tatizo la wahamiaji si kutafuta manusura baharini, bali kuwakabili mawakala hao wa kusafirisha watu, akiwaita wafanyabiashara wa watumwa wa leo. Ametaka kikao cha umoja wa ulaya ndani ya wiki moja kujadili tatizo hili kubwa.
Papa Francis kwenye misa ya Jumapili alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua ya haraka kuepuka janga lingine kama hilo.
Meli pamoja na helikopta za Italia na Malta ziliendelea na shughuli ya kusaka miili usiku kucha. Mamlaka za Sicily zinasema wengi wa abiria kwenye boti iliyozama walikuwa ni kutoka mataifa ya Algeria, Misri Somalia, Senegal na hata Zambia.
Friday, 17 April 2015
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameitaka timu yake kutafuta ushindi wa mapema katika pambano la mwishoni mwa wiki hii Jumamosi dhidi ya Reading. Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa vijana wake wanapaswa kuanza kwa kasi na nguvu katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Wembley kama kweli wanahitaji kutetea taji lao.
Wenger amesema kwamba timu yake imejifunza msimu uliopita ambapo walihitaji penati kuishinda Wigan katika hatua ya nusu fainali kabla ya kutanguliwa goli mbili na wapinzani wao Hull City katika pambano la fainali ambapo hadi mwisho wa kipute hicho, waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2.
Mechi hiyo itakuwa ni nusu fainali ya kumi kwa mzee Wenger ,huku akidai kwamba Arsenal inajiamini hasa kutokana na kushinda mechi nane mfululizo. Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili ambapo Aston Villa itawakaribisha Liverpool.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
atika hukumu nadra kutolewa nchini Tanzania, mahakama Kuu Kanda ya Tabora imeiagiza halmashauri ya wilaya ya Urambo, kulipa fidia ya shilingi milioni 25 kwa Mwamini Adam na mumewe Idrisa Jafari kutokana na madhara waliyopata baada ya uzembe uliofanywa na daktari wa hospitali ya wilaya hiyo alipokuwa akimfanyia upasuaji Mwamini.
Katika uamuzi wa shauri hilo la madai Namba 13/2011 uliotolewa hivi karibuni, Mahakama Kuu imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Mwamini shilingi milioni 20 kutokana na kilema alichopata kwa kuondolewa mfuko wa uzazi na kukatwa utumbo. Pia, mahakama imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Jafari fidia ya shilingi milioni tano ikiwa ni gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
Akisoma hukumu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amir Mruma alikubaliana na madai ya walalamikaji kuwa madhara waliyopata kutokana na uzembe uliofanywa na Dk Jackob Kamanda ni makubwa.
Jaji Mruma alisema haipingiki kwamba huo ni uzembe uliofanywa na mtumishi, hivyo mwajiri anapaswa kulipa gharama.
Aliagiza kuwa kiwango hicho cha fedha kitalipiwa riba ya asilimia saba kila siku kuanzia tarehe ya uamuzi ulipotolewa hadi siku mlalamikiwa atakapolipa fedha hizo.
Mwamini na mumewe walifikisha malalamiko yao Mahakama Kuu, wakidai kulipwa fidia ya shilingi milioni 505 kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wakati wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mgonjwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Anatory Lukonge wa Hospitali ya Itigi ambako walibaini kitambaa tumboni mwa Mwamini, aliieleza mahakama kuwa walipomfanyia upasuaji walikuta utumbo umeshikana na kizazi huku juu yake kukiwa na kitambaa.
Dk Lukonge alisema walikitoa kitambaa hicho lakini kutokana na sehemu ya kizazi kuharibika, iliwalazimu kukiondoa huku akidai kuwa hali hiyo ilisababishwa na uzembe wa daktari aliyemfanyia upasuaji.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Mapigano yanaendelea kuwania udhibiti wa mji wa Ramadi nchini Iraq kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa Islamic State.
Majeshi yanayoongozwa na Marekani yamefanya mashambulio ya anga dhidi ya vijiji vitatu ambavyo vilikuwa vimetwaliwa na majeshi ya Islamic State Jumatano.
Majeshi ya serikali ya Iraq mjini Ramadi pia yameripotiwa kupambana na wapiganaji wa I-S.
Maelfu ya watu wanakimbia mji wa Ramadi wakati huu mapiganao yanapopamba moto.
Kiongozi mmoja wa kisiasa wa eneo hilo Farhan Mohamed wa baraza la jimbo la Anbar ameishutumu serikali ya Iraq inayodhibitiwa na waumini wa madhehebu ya Kiislam ya Shia kwa kulitelekeza jimbo la Anbar wakati likiwa katika mapigano makubwa.
Jimbo la Anbar, wakazi wake wengi ni wa madhehebu ya Sunni.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
viongozi wa vyama vitano vya upinzani wameshiriki katika mdahalo wa pili wa moja kwa moja ulioandaliwa na BBC.
Katika hoja za kwanza, kiongozi wa chama cha Labour, Ed Miliband, amesema suala la familia za wafanyakazi atalipa kipaumbele kwanza, wakati kiongozi wa UK Independence Party,UKIP, Nigel Farage amesema atasaidia biashara ndogo ndogo. Nicola Sturgeon kiongozi wa chama cha Scotish National Party amesema anataka kuona muungano wa Uingereza unakuwa bora zaidi katika kila sehemu ya nchi hiyo. Viongozi wa Plaid Cymru na Green Party pia nao wameshiriki katika mdahalo huo.
Bwana Miliband, amesema anatarajia kupata ushindi mkubwa na hataunda serikali ya mseto na chama cha SNP.
Wagombea hao wamekuwa wakipingana katika masuala mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
Waziri mkuu David Cameron wa chama tawala cha Conservatives na naibu waziri mkuu wake kutoka chama cha Lib Dem, Nick Clegg hawakushiriki katika mdahalo huo wa wazi.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limetoa kanda yenye ushahidi inayoonyesha matumizi ya gesi ya chlorine kwenye shambulizi moja mwezi uliopita nchini Syria.
Kanda hiyo inaonyesha watoto watatu walio chini ya miaka minne ambao walikufa licha ya kuwepo jitihada za kuwakoa.
Daktari raia wa Syria ambaye aliwatibu watoto hao kwenye hospitali moja iliyo mkoa wa Idlib aliuambia mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kumekuwa na visa kadha vya mashambulizi ya gesi mwezi mmoja uliopita.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power anasema kuwa ni serikali tu ya rais Bashar al-Assad iliyo na helkopta zinazotumiwa kudondosha mapipa yenye milipuko iliyo na kemikali hatari.
Awali serikali ya Syria imekana madai hayo ikayataja kuwa propaganda.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda baadaye.
Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa.
Rais Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi.
Thursday, 16 April 2015
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Huku ujenzi wa ua utakaotenganisha Kenya na Somalia ukianza kwa madhumuni ya kuwakomesha wanamgambo wa Al Shabaab kutoishambulia Kenya,
shirika la BBC limepata ushahidi kuwa kundi hilo lenye makao yake nchini Somalia linaendelea kuwasajili wanachama wapya katika miji mikuu ya Kenya.
Katika mji wa Isiolo ulioko Kaskazini Mashariki mwa Kenya, takriban vijana barubaru 26 wametoweka makwao.
BBC imebaini kuwa vijana hao wamewapigia wazazi wao simu wakiwaarifu kuwa tayari wamejiunga na wanamgambo wa Al Shabab.
Nusu ya wazazi wao wameripoti kutoweka kwao kwa vyombo vya usalama .
Asilimia kubwa ya wale waliokaa kimya wanahofia kudhalilishwa na maafisa wanaopambana na ugaidi nchini Kenya .
Ilikuwashawishi wakenya kujiunga na serikali kutambua wafuasi wa kundi hilo waliotangamana na jamii, serikali ya Kenya imetangaza
msamaha kwa wakenya waliojiunga na Al Shabaab maadamu watajisalimisha kwa vyombo vya dola katika kipindi cha siku 10 zilizotolewa.
Matukio haya yanawadia takriban majuma mawili tangu wapiganaji wa kundi hilo kuivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua takriban wanafunzi wakristu 150.
Serikali ya Kenya baadaye ilitangaza kuwa kiongozi wa wapiganaji hao alikuwa ni Wakili mkenya.
Usajili huu unaoendelea unatizamwa na wachanganuzi wa maswala ya kiusalama kama mbinu mpya na ya kuhofiwa.
Ukweli ambao umewaogofya wabunge na maafisa wa usalama nchini humo.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa kiislamu wanaoheshimiwa nchini Kenya Sheikh Abdullahi Salat, ameonya kuwa hofu ya jamii dhidi ya polisi na shauku huenda ikahujumu jitihada hizo.
Serikali imepuzilia mbali maoni hayo ikidai kuwa ni kisingizio tu.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Marekani itaanda mashindano ya riadha duniani kwa mara ya kwanza mwaka 2021.
Mji wa Eugene katika jimbo la Oregon ulichaguliwa na shirikisho la riadha duniani IAAF.
Shirikisho hilo lilikiuka sheria za utoaji zabuni.
IAAF limesema kuwa uamuzi huo ni mpango uliofanywa baada ya Gavana wa jimbo la Oregon pamoja na kamati ya Olimpiki ya Marekani kutoa usaidizi wa kifedha.
Mji wa Eugene ulishindwa katika harakati zake zaa kuandaa mashindano hayo mwaka 2019 baada ya mashindano hayo kukabidhiwa mji wa Doha nchini Qatar.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.
Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani.
Danielle Busby ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao wamepewa majina ya Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige;anasema kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya juu.
Inasemekana watoto wengi sawa na hao walihahi kuzaliwa mara moja huko London Uingereza ,mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.
Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada ilikumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao ambao hawakuwa wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji .
Baba wa mtoto huyo, Adam Busby amewamiminia sifa kedede wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni hiyo.
Bwana Busby amesema kuwa mwanawao wa kwanza Blayke anawasubiri kwa hamu na ghamu.
Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi kwa mimba zake zote mbili.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Mechi za klabu bingwa barani Ulaya katika hatua ya robo fainali ziliendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo miwili kupigwa. Bayern Munich walikuwa ugenini kukipiga na FC Porto ya Ureno. Katika hali isiyotarajiwa na wengi Bayern imeangukia pua kwa kucharazwa mabao 3-1.
Nako nchini Ufaransa wenyeji Paris Saint German ilishuka dimbani kuikabili miamba ya soka ya Hispania Barcelona. Katika mchezo huo wenyeji PSG wamejiweka katika hali ngumu baada ya kucharazwa mabao 3-1. Bao la Neymar jr na mawili ya Luis Suárez yalitosha kuwazamisha wenyeji wao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Timu zote nne zitacheza michezo ya marudiano April 21 siku ya Jumanne.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Katika hali isiyotarajiwa bondia raia wa Marekani Floyd Mayweather ameamua kufanya mazoezi ya wazi na kuruhusu vyombo vya habari kuchukua picha ikiwa ni maandalizi kuelekea katika pambano lake dhidi ya bondia Manny Pacquiao raia wa Philippine.
Mayweather ambaye ni bingwa wa WBA na WBC, ameweka rekodi ya kucheza mapambano 47 ya kulipwa bila kupoteza hata moja wakati mpinzani wake amepigana mapambano 57, akiwa amepigwa mara tano na kutoka sare mara mbili.
Pambano kati ya wawili hao linatarajiwa kufanyika mnamo May 2 mwaka huu, huku pigano hilo likitajwa kuwa ndio la pesa nyingi zaidi katika historia ya ngumi duniani.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Jaribio la kwanza la ndege inayotumia umeme jua limefanyika leo baada ya ndege hiyo kufanikiwa kuanza kuruka asubuhi ya leo.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Katika tukio hilo, mmoja anayesadikiwa kuhusiana na watu hao waliokamatwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa panga askari polisi aliyekuwa akipambana naye.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.Kamanda Paul alimtaja mtu aliyefariki kuwa ni Hamad Makwendo ambaye umri wake haujafahamika ambaye ni mkazi Manyasini Ruaha wilayani Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Paul alisema: “Polisi walipata taarifa kuwa watu hao walitumia usafiri wa bajaji mbili kwenda kusikojulikana na wakati wakiendelea na zoezi la kufuatilia ndipo walikutana na bajaji moja ikiwa na abiria mmoja ambaye ni Mkwendo na kuisimamisha.”
Alisema kuwa bajaji hiyo iliposimama marehemu huyo aliruka na kuanza kukimbia ndipo askari mwenye namba F .3323 Koplo Nasoro alianza kumkimbiza na alipomkaribia mtuhumiwa huyo alichomoa jambia alilokuwa nalo na kumkata askari huyo eneo la shingoni.
Askari mwingine mwenye namba E.9245 Koplo Chomola ambaye alikuwa nyuma alifanikiwa kumpiga risasi ya mguu mtuhumiwa huyo, ambapo alipoanguka chini wananchi wa eneo hilo tayari walifika katika eneo hilo na kuanza kumshambulia marehemu huyo kisha kumchoma moto kwa hasira.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu wengine ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka.”
Alisema polisi walendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni.
Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokutwa katika mabegi yaliyokuwa ndani ya msikiti huo ni pamoja na milipuko 30, bendera nyeusi yenye maandishi ya Kiarabu yakisomeka ‘Mungu Mmoja’, majambia, bisibisi, vinyago vya kuziba uso (masks), nguo za jeshi, misumeno ya chuma na spana.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Mwaandishi habari mmoja raia wa Lebanon leo atakuwa mshtakiwa wa kwanza kufikishwa kizimbani katika mahakama ya jinai ya ICC iliyoko The Hague nchini Uholanzi katika uchunguzi wa kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri.
Bi Karma Khayat na runinga anayoifanyia kazi ya Al-Jadeed, yanashutumiwa kwa kupuuza ushauri wa kundi maalum la uchunguzi wa kesi hiyo nchini Lebanon, kwa kutoa taarifa kuwahusu mashahidi.
Amekanusha kutenda kosa lolote.
Bi Khayat amesema kuwa ripoti yake ilikuwa kwa manufaa ya uma.
Mahakama hiyo maalum ilibuniwa na umoja wa mataifa, ili kubaini watu waliohusika na mauaji ya bwana Hariri.
Watu watano wanaotuhumiwa kuhusika katika mauwaji hayo ya Hariri wangali mafichoni.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Maelfu ya raia katika mji wa mashariki wa Durban nchini Afrika Kusini wanaandamana kupinga ghasia za hivi majuzi dhidi ya wageni.
Takriban watu watano wameuawa tangu wiki iliopita katika ghasia dhidi ya wahamiaji ambao wameshtumiwa kwa kuchukua kazi za raia wa taifa hilo.
Hofu ya kusambaa kwa ghasia inaendelea kutanda.
Mjini Johannesburg ,wamiliki wa maduka kutoka mataifa ya Ethiopia,Somalia na mataifa mengine ya Afrika wamefunga biashara zao wakihofia kuporwa.
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini ameshtumu ghasia hizo na anatarajiwa kulihutubia bunge baadaye.
Mnamo mwaka 2008 watu 62 waliuawa kufuatia ghasia za kibaguzi zilizokumba taifa hilo.
![](http://1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
![](http://2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mandera kazkazini mwa Kenya wanasema kuwa takriban watu 35 wametoweka baada ya basi kusombwa na mafuriko kilomita chache kutoka mji huo.
Mvua kubwa iliripotiwa kunyesha katika eneo la mji huo na viunga vyake mapema Alhamisi.
Maafisa wa msalaba mwekundu wanasema wamewaokoa watu 30
Basi hilo liliondoka mjini Mandera likielekea jijini Nairobi mapema siku ya jumatatu kabla ya kukwama katika matope.
Baadaye mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kulisomba basi hilo.
Maafisa wa msalaba mwekundu wanasema kuwa wameanza kuwasaka watu waliotoweka katika mto mmoja uliopo ambapo mafuriko hayo yanaelekea.
Subscribe to:
Posts (Atom)