Tuesday, 2 June 2015


Kilabu ya Manchester United inaamini iko katika nafasi nzuri ya kumsajili Dani Alves kutoka Barcelona iwapo kocha Louis Van Gaal anataka kumsajili beki huyo wa kulia.
Alves atakuwa hana mkataba mwishoni mwa msimu huu na Barcelona iko tayari kumwachilia beki huyo wa miaka 32 kuondoka baada ya mechi ya fainali ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Juventus siku ya jumamosi mjini Berlin.
Klabu ya PSG pia inamuania Alvez ijapokuwa kocha wake Laurent Blanc anaamini mchezaji huyo bado anataka kusalia Barcelona.
Lakini maoni ya Old Trafford ni kwamba Alvez hangependelea kujiunga na PSG.
Dani Alves
Van Gaal anapanga kumsajili beki wa kulia.Licha ya umri wake mkubwa ukosefu wa fedha za uhamisho zinamfanya mchezaji huyo kuwa muhimu.
Mchezaji huyo wa Brazil anapokea kitita cha pauni 120,000 kwa wiki, fedha ambazo United inaweza kuzilipa bila kutoa jasho.

Shirikisho la kandanda duniani,FIFA, limekanusha madai kwamba katibu wao mkuu,Jerome Valcke,alihusika katika kashfa ya ufisadi ambapo hongo ya mamilioni ya dola ilitolewa.
Kashfa hiyo inachunguzwa na Marekani .
FIFA inasema hamna afisa wake yeyote wa ngazi ya juu aliyehusika kwa njia yoyote katika kashfa hiyo.
Jerome Valcke
Inasemekana malipo hayo ya rushwa yalitolewa na serikali ya Afrika Kusini kwa maafisa wa soka wa huko Marekani ili waunge mkono wenzao Waafrika walio ng'ambo katika nchi ya visiwa vya Caribbean.
Waendesha mashtaka wa Marekani wanasema hongo hiyo ilinuiwa kusaidia kununua kura kuiwezesha Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa kombe la dunia lililofanyika mwaka 2010.

Wanamgambo wa kiislamu nchini Nigeria wametoa picha mpya za video lakini Kiongozi wa Boko Haram ambaye huwa anaonekana kwenye video zao, Abubakar Shekau hakuonekana kwenye picha hizo za video.
kutoonekana kwa Shekau kwenye Video hiyo kumeleta hali ya wasiwasi kuhusu kuwepo kwa hali ya mgawanyiko ndani ya kundi hilo.
Takriban watu 13 wameuawa siku ya jumanne katika shambulio la bomu katika Soko la Ng'ombe mjini Maiduguri, mji ambao uliwahi kuwa ngome ya Boko Haram, Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Katika picha ya video ya dakika 10, msemaji huyo amekanusha taarifa zilizotolewa na Jeshi la Serikali kuwa linadhibiti miji yote kutoka mikononi mwa wanamgambo.
Ameonyesha vitambulisho vya wanajeshi akisema kuwa wameuawa, na kuonyesha mabaki ambayo amedai ya ndege ya kijeshi waliyoidungua.
Msemaji aliyekuwa amebeba bunduki na huku uso wake ukiwa umefunikwa, amesema video hiyo ilirekodiwa sambisa, msitu unaozunguka hifadhi.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari,amesema kuwa vikosi vya kijeshi viko kwenye doria mjini Maiduguri na kuhakikisha kuwaondoa wanamgambo hao katika eneo hilo.
Baadae wiki hii, Buhari atakutana na Viongozi wenzie wa nchi jirani kwa ajili ya kuzungumzia mikakati ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu.
Takriban watu milioni moja na nusu wamekimbia makazi yao, na mamia zaidi wametekwa tangu kuanza kwa harakati za kundi hilo mwaka 2009.
Zaidi ya Watu 15,500 wameuawa katika mapigano.
Rafael Nadal bingwa mara tisa wa michuano hiyo anavaana na Djokovic mchezaji nambari moja kwa ubora. Nadal Mhispania amewahi kumshinda Mserbia Djokovic mara sita katika michuano hiyo siku za nyuma.
Huu unaelezwa kuwa mpambano mkali zaidi katika michuano ya French Open inayoendelea katika viwanja vya tenis mjini Paris ukiwemo uwanja wa Roland Garros.
Rafael Nadal
Mchezaji nambari mbili kwa ubora katika mchezo huo duniani kwa wanaume na bingwa wa mwaka 2009 Roger Federer ameng'olewa katika michunao hiyo hatua ya robo fainali baada ya kucharazwa na Stan Wawrinka kwa seti 6-4 6-3 7-6 (7-4).
Wawrinka, mwenye umri wa miaka 30, amewahi kupoteza michezo yote minne walipokutana na Federer katika michuano hiyo mikubwa.
Lakini Wawrink ambaye ni wa nane kwa ubora katika tenis amemwangusha Federer mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa mchezaji mwenza katika michuano ya Kombe la Davis.
Andy Murray
Kwa matokeo hayo Wawrinka atapambana hatua ya nusu fainali na Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga ambaye anapewa nafasi kubwa kufuatia ushindi wake dhidi ya Mjapan Kei Nishikori.
Tsonga alipata kibarua kigumu kumng'oa mpinzani wake Nishikori alipopata matokeo ya kufunga seti tatu dhidi ya mbili yaani 6-1 6-4 4-6 3-6 6-3.
Kwa upande mwingine Andy Murray leo atajaribu kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya French Open kwa mara ya tatu katika siku ambayo Novak Djokovic na Rafael Nadal wanapambana mjini Paris.
Murray wa tatu kwa ubora duniani anacheza dhidi ya Mhispania David Ferrer anayeshika nafasi ya saba kwa ubora.
Murray amesema hilo litakuwa pambano kali na mtihani mkubwa kwake.

Waziri wa Usafirishaji wa China amesema wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanawapata watu walionusurika miongoni mwa mamia ya waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa meli katika mto Yangtze kutokana na hali mbaya ya hewa.
Maelfu ya waokoaji walifanya kazi usiku kucha katika meli hiyo iliyopinduka ijulikanayo kama "Nyota ya Mashariki" katika jimbo la Hubei.
Watu saba wamethibitika kufa na wengine 14 wamekutwa hai katika meli hiyo iliyokuwa na watu 456.
Ndugu waliojawa na hasira wanalalamikia kukosekana kwa taarifa za uokoaji.
Watu walionusurika ni pamoja na nahodha wa meli na mhandisi mkuu, wote wawili wakiwa katika mahabusu za polisi.
Nahodha amesema meli hiyo ilikumbwa na kimbunga na kuzamishwa chini ya mto katika dakika chache.

Imeripotiwa kuwa Raisi wa Fifa,Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili kuthibitisha tuhuma za rushwa zinazomkabili vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Wakati ambao waendesha mashtaka nchini Marekani wanaoifuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa Fifa nchini Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa.
Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema kuwa bado maafisa hao wa marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa chafu unavyomuhusisha Blatter.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa uchunguzi na si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini Marekani na mwanasheria wa New York , ambaye alishiriki katika uchunguzi huo walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.

Tuesday, 26 May 2015


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.
Papa Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.
Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutizama runinga kwa miaka 25 sasa.
Isitoshe raia huyo wa Argentina amesema kuwa hatumii mtandao wa intaneti.
Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano.
Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu
Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.
Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?

Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246
"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.
Wenyeji wameshauriwa kukaa ndani na kunywa maji mengi
Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.

Klabu ya soka ya England Norwich City imefanikiwa kurejea katika ligi kuu ya nchi hiyo baada ya kuibanjua Middlesbrough kwa jumla ya bao 2-0.
Bao la Cameron Jerome na Nathan Redmond,yalitosha kabisa kuipa ubingwa Norwhich na kunyakua kiasi cha paundi million 120 kwa ushindi huo na kutinga ligi kuu almaarufu EPL.
Katika mtanange huo uliopigwa katika dimba la Wembley, takribani mashabiki elfu thamanini na tano walikuwepo uwanjani wakishuhudia vijana hao wa mji wa Norwich wakirejea tena ligi kuu na kuungana na wenzao Bournemouth na Watford ambazo tayari walishakata tiketi.

Bosi wa timu ya Mercedes Toto Wolff ametanabaisha kuwa dereva wa timu hiyo Lewis Hamilton ataerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupata mfadhaiko uliotokana na matokeo mabaya katika mashindano ya Monaco Granda Prix.
Hamilton alijikuta akiangukia nafasi ya tatu mwishoni mwa wiki iliyopita japo kuwa anguko lake lilisababishwa na matatizo ya kiufundi katika gari alilokuwa analiendesha. ''ana hilo tatizo la msongo wa mawazo, na yupo katika harakati za kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Inaumiza sana kupoteza mchezo ule kwa sababu ushindi ulikuwa wake, lakini sina shaka kwamba atarejea haraka kama afanyavyo siku zote" alisema bosi huyo. Mwenyewe Hamilton amesema hakuna wa kumlaum kwasababu wanafanya kazi kama timu. Kwenye ushindi huwa wote na kwenye kushindwa pia huwa wote.

Hatimaye miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.
Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya. Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.

Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano mjini Bujumbura
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.

Askari mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa Kenya
Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa alshabaab katika kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.Msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka ameiambia BBC kuwa kulikuwa na makabiliano makali kati ya Polisi na wapiganaji hao.
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo. Polisi wameiambia BBC kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama.
Taarifa za awali zilieleza kuwa askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo al shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa.Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara 

Thursday, 14 May 2015


Michuano maarufu ya riadha duniani ya Diamond League inaanza Doha,Qatar mwishoni mwa wiki hii, huku wakimbiaji nguli kutoka nchi mbakimbali ikiwemo
Kenya kushiriki.Kwa mara ya kwanza katika historia, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000, Mo Farah kutoka Uingereza naye atashiriki
huku akisema kuwa anategemea upinzani mkubwa kutoka kwa washiriki.Miongoni mwa wanariadha kutoka Kenya wanaotegemewa kushiriki ni pamoja
na Edwin Soi, Thomas Longosiwa na Isaiah Kiplangat Koech .Soi ni mshindi wa medali ya shaba wa mita 5,000 katika michuano ya
Olimpiki ya mwaka 2008 iliyofanyika Beijing, China, wakati Longosiwa naye ni mshindi wa medali ya shaba wa Olimpiki ya London.
Kiplangat ni mshidni wa dunia wa mita 5,000 wa medali ya shaba.Yenew Alamirew na Hagos Gebrhiwet kutoka Ethiopia wanategemewa pia
kushirik iakiwemo mwana dada Allyson Felix kutoka Marekani.Waandaaji wa michuano hiyo wametenga dola milioni nane kwa ajili ya zawadi.

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaendelea na mazoezi mepesi mjini Rustenburg, Afrika Kusini tayari kwa michuano ya Kombe la
COSAFA inayoanza Jumapili.Timu hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki na Watanzania waishio Afrika ya Kusini.
Michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Stars tayari kuivaa The Cranes ya Uganda katika mechi ya awali ya michuano ya CHAN (kwa
wachezaji wa ndani).
Kocha wa Stars, Mart Nooij amesema michuano hiyo itaiweka vema Stars kwa ajili ya CHAN na michuano ya AFCON ya 2017.
Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng, ikishirikisha
nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
Nooij, kuelekea katika michuano hiyo, amewaacha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya watu wa
Congo, Mbwana Samatta na Thomasi Ulimwengu. Kikosi cha Stars kilichopo Afrika ya Kusini kinajumuisha wachezaji wafuatao.
Makipa: Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Mwadini Ali (Azam), mabeki
ni Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua,
Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na
Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM).
Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam), Said Juma,
Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba) na Mwinyi
Kazimoto (Al Markhiya, Qatar).
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba), Mrisho Ngassa (Free State
Stars), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (Zeco
United).
Kutoka kulia Erasto Nyoni, Msuva, Shomary Kapombe na Hassan Dilunga

Wakuu wa mambo ya kale nchini Syria wameonya juu ya majanga yanayosababishwa na kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislamu, Islamic State nchini humo baada ya kuukamata mji wa Palmyra, ambao ni miongoni mwa miji iliyotengwa kuwa uridhi wa dunia ulioko Mashariki ya Kati.
Wanamgambo hao wa IS wanaelezwa kukamata vijiji kadhaa vilivyo jirani na mji huo wa Palmyra na wamekwisha kuwaua wana vijiji zaidi ya ishirini wengi wao waliuawa kwa kukatwa vichwaa .
Mji huo wa Palmyra ni miongoni mwa miji inayohifadhiwa kutokana na historia yake nalo shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni ,UNESCO limekwisha kuutangaza mji huo kuwa hifadhi ya uridhi kwa dunia.
Kundi hilo la IS bila ya kujali wamekuwa waki haribu maeneo ya hifadhi za namna hiyo kama walivyo fanya nchini Iraq.
Palmyra nayo imekwisha kukabiliana na uharibifu huo wakati wa vita nchini Syria uliosababishwa na mgogoro wa kiraia dhidi ya serikali yao baada ya vikosi vya serikali kuweka kambi katika maeneo kama hayo ambayo ni urithi wa dunia.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini Tanzania saa moja baada ya kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi mkuu wa majeshi yake Meja jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba amempindua.
Jenerali huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa kiwanja cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata hivyo haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono generali Meja jenerali Godefroid Niyombare.naye msemaji wa rais wa Burundi ,amesema kwamba wanajeshi watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa viongozi nchini Tanzania,amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na watutsi ,vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa. lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa na masuala ya ukabila.
Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe .


Katika kile kinachoonekana ni kuweka mikakati ili kuchukua ubingwa msimu ujao, wekundu wa Msimbazi, Simba inahaha kutafuta wachezaji
kutoka nje ya nchi ili kuimarisha kikosi chake.
Hatua hiyo inakuja baada ya Simba, iliyomaliza ya tatu katika msimu wa
ligi iliyopita, kuripotiwa kuachana na wachezaji watatu wa kigeni kutoka Uganda, Simon Sserunkuma, Dan Sserunkuma na Joseph Owino
kufuatia pendekezo la kocha Mserbia Goran Kopunovic.Habari kutoka Simba zinasema sasa ni wakati wa kutafuta wachezaji
katika nchi jirani za Afrika ili kuziba pengo la Waganda hao.
Baachi ya nchi ambazo zimeelezwa kuwa Simba inasaka wachezaji ni
pamoja na Ghana, Nigeria, Rwanda, Burundi na Kenya.Uamuzi huo unakuja baada ya Simba kuwe nje ya michuano ya kimataifa
kwa takriban miaka mitatu mfululilizo.Ligi kuu ya Tanzania Bara imekwisha hivi karibuni huku Yanga ikiwa
bingwa na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam kumaliza nafasi ya pili.
Yanga na Azam ndio wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya
vilabu ya CAF hapo mwakani.Yanga itashiriki kombe la Washindi barani Afrika na Azam itashiriki kombe la Shirikisho.


Mwaandishi wa habari wa BBC katika eneo la baharini huko Andaman katika pwani ya Thailand ameshuhudia mateso makubwa wanayopitia wahamiaji.
Maboti zaidi yanayowabeba wahamiaji walio na matatizo chungu nzima, yamekwama katika bahari huko Andaman, kutokana na hatua ya serikali ya Thailand, Malaysia na Indonesia kufunga mipaka ya nchi zao.
Wahamiaji hao wameachwa baada ya Thailand kuwatimua walanguzi wa watu kutoka katika bahari ya nchi hiyo.
Maelfu ya wahamiaji hao ni kutoka katika kabila dogo la Rohingya - kabila linalodhulumiwa na utawala wa Myanmar.
Wahamiaji
Phil Robertson ni naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch -- anasema kuwa hata ingawa hali ya kisheria kwao bado ina ati ati, wengi wa walioko kwenye maboti hayo hawana maji wala chakula.
Radio na Runinga ya taifa inanganganiwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkrunziza ndio wanaoidhibiti.


Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda.
Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC.
Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku.
Waasi wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanyana mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni.
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu.
ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na ndo, panga na visu.

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
21.15pm:-Nkurunziza hayuko Tanzania,Je Yuko wapi?Msemaji wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe amezungumza na mwandishi wetu na kuthibitisha kuwa Nkurunziza aliondoka nchini Tanzania siku ya jumatano lakini hawezi kubaini iwapo yuko nchini Burundi au la.Amesema kuwa kutokana na maswala ya usalama hawezi kutaja mahala alipo lakini yu buheri wa afya.
20.25pm-Jenerali Godefroid Niyombare
Jenerali Godefroid
Jenerali aliyetangaza mapinduzi .
20.28pm-Wanajeshi watiifu wa Nkurunziza
Mji wa Bujumbura
Wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza wametangaza kudhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu wa Bujumbura siku moja baada ya jaribio la mapinduzi.Kulikuwa na mapigano makali mjini Bujumbura,hususan katika kituo cha habari cha kitaifa,lakini makabiliano hayo yameisha huku wanajeshi watano wakidaiwa kuuawa.
18.05pm-Wanajeshi watiifu
Wanajeshi watiifu wapiga doria Bujumbura
Makundi hasimu ya jeshi la Burundi yamekuwa yakipambana kukidhibiti chombo cha kitaifa cha habari RTBN ambacho kilizimwa kwa mda .Duru zimearifu kuwa kituo hicho cha habari kiko chini ya udhibiti wa vikosi vinavyomtii rais Pierre Nkurunziza.
17.53pm-Viongozi wajadili Burundi
Baraza la usalama la umoja wa Afrika laijadili Burundi kwa sasa
Baraza la usalama la umoja wa Afrika limetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter likisema kuwa wanachama wa baraza hilo kwa sasa wanaijadili.
17.00pm-Wanajeshi wapiga doria
Maafisa wa polisi wapiga doria Burundi
Maafisa wa polisi waliojihami katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wanaonekana wakilinda vizuizi vya barabarani leo
16.50pm-Mkutano kuhusu Burundi waendelea.
Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika
Baraza la usalama la umoja wa Afrika kwa sasa linaijadili Burundi.
tweets: "Chini ya Uongozi wa balozi Amina Diallo wa Niger,ni mkutano wa 507.Baraza hilo linaangazia hali ilivyo Burundi
16.10pm-RNTB yarudisha matangazo
Kituo cha redio
Kituo cha redio cha Burundi RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa kimeanza kurusha tena matangazo.
15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusamehe
Ris wa Burundi Pierre Nkurunziza
Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.
15.47pm-Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi
Ramani ya taifa la Burundi.
15.45pm-Mji wa Bujumbura
Burundi
Mji wa Burundi Bujumbura ulivyo kwa sasa
15.30pm-Vyombo vya habari vyazimwa
KItuo cha habari cha Isanganiro
Kituo cha habari cha Burundi Isanganiro kimesema kuwa kimefungwa na vituo vyengine vya kibinafsi .Kituo hicho ni miongoni mwa vile vilivyotangaza mapinduzi siku ya jumatano.
15.17pm-Kituo cha habari
Askari Burundi
Kituo cha habari cha Redio ya RTNB kimezimwa kufuatia mapigano makali karibu na afisi zake mjini Bujumbura.
15.01pm:Rais wa Burundi Ahojiwa
Wanajeshi nchini Burundi wakipiga doria
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
14.30pm:Makundi ya vijana waliojihami
Vijana Burundi
Kuna madai kwamba kundi la vijana linalunga mkono serikali limeshambulia kituo kimoja cha habari cha kibinafsi mjini Bujumbura.KUndi hilo linalojulikana kama Imbonerakure,baadhi ya watu wanaamini kwamba vijana hao wanatumiwa kama wapiganaji na kwamba huenda wamepewa silaha ili kuwatishia raia kabla ya uchaguzi.
13.45pm-Hali ni tete Burundi
Wanajeshi wa BUrundi
Hali bado ni tete nchini Burundi siku moja tu baada ya jenerali mmoja wa jeshi kujaribu kutekeleza mapinduzi .Barabara nyingi zimeendelea kuwa bila watu kwa kipindi kirefu cha alfajiri huku wengi wakisalia ndani ya majumba yao wakihofia usalama kulingana na mwanahabari wetu Ruth Nesoba.
13:30pm-Ukabila
Kiongozi wa jeshi aliyetangaza mapinduzi
Tofauti zilizopo katika jeshi la Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi hazionekani kuwa katika misingi ya kikabila ,mkuu wa majeshi ambaye ni mtiifu kwa rais Nkurunziza pamoja na jenerali wa majeshi aliyetangaza mapinduzi hayo ni wa kabila la Hutu.Makundi hayo yanaonekana kugawanyika kati ya wale wanaoamini rais Nkurunziza alikiuka makubaliano ya amani yaliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu na wale wanaosalia kuwa watiifu kwake
12:05pm-Wanajeshi watiifu
Mj wa Burundi Bujumbura
Afisa mmoja wa kijeshi ameiambia BBC Afrique kwamba wanajeshi watiifu nchini Burundi wanadhibiti mji wa Bujumbura ,uwanja wa ndege,makao ya rais pamoja na vituo vya redio na runinga.
12:00pm-Milio ya Risasi
Wanajeshi wa Burundi
Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika